Latest News & Events

ACCT wamejenga Kisima no 452 katika kitongoji cha Ipanga

Chama cha Makandarasi wazalendo Tanzania (ACCT) kwa kushirikiana na kampuni ya Afro Supplies Ltd, ili kumuenzi Mzee Mahamudu Jessa aliyekuwa mkurugenzi wa Afro Supplies Ltd kama kumbukumbuku na thawabu; wamejenga Kisima no 452 katika kitongoji cha Ipanga, kijiji cha Nyabubinza kata ya Mataba, Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu.