ACCT wamejenga Kisima no 452 katika kitongoji cha Ipanga

Error message

Deprecated function: The each() function is deprecated. This message will be suppressed on further calls in _menu_load_objects() (line 579 of /home/acctco/public_html/includes/menu.inc).
Chama cha Makandarasi wazalendo Tanzania (ACCT) kwa kushirikiana na kampuni ya Afro Supplies Ltd, ili kumuenzi Mzee Mahamudu Jessa aliyekuwa mkurugenzi wa Afro Supplies Ltd kama kumbukumbuku na thawabu; wamejenga Kisima no 452 katika kitongoji cha Ipanga, kijiji cha Nyabubinza  kata ya Mataba, Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu.
 
Wakazi wa eneo hilo wameshukuru sana kwa ukombozi huu wa kujengewa kisima cha maji ambacho kitahudumia idadi kubwa ya wakazi takribani watu 520 kutoka kaya 75 ambazo zilikuwa zikihangaika sana kupata maji safi na salama kwa matumizi yao ya kila siku.