NAFASI ZA MAFUNZO KWA MAFUNDI

Error message

Deprecated function: The each() function is deprecated. This message will be suppressed on further calls in _menu_load_objects() (line 579 of /home/acctco/public_html/includes/menu.inc).

Chama cha Makandarasi (ACCT) kilifanya utafiti na kubaini  baadhi ya mapungufu  katika kandarasi  za wazawa  ambazo zinasababisha makandarasi hawa  kushindwa kuhimili ushindani na   kampuni za makandarasi  kutoka nje, sababu  mojawapo ni ujuzi  na uelewa mdogo wa Mafundi ambao ndio watekelezaji wa kazi hizo. Mbali na kufanyakazi kwa mazoea, mafundi hawa hukosa taaluma sahihi kwenye fani yao ili kutekeleza majukumu yao kwa  ufanisi unaotakiwa ili kuhimili soko la ushindani kwani walio wengi wamejifunza kazi wakiwa site.

Kwa kutambua hili Chama cha Makandarasi Wazalendo Tanzania (Association of Citizen Contractors Tanzania- ACCT)  Kimeanzisha kituo cha mafunzo kilichopo Arusha Technical College, kwa kushirikiana na taasis ya Netherland iitwayo PUM wanatoa mafunzo ya muda mfupi (wiki mbili)  kwa Mafundi wa fani mbalimbali, ikiwemo plastering, Tiles Layer, Painting, Plumbing  n.k  ambayo hutolewa katika misimu tofauti. Mafundi hawa hupitia madaraja matatu kabla ya kukamilisha  mafunzo haya ambapo mbali na kongeza ujuzi katika taaluma yao pia wanakuwa waalimu wazuri kwa wenzao katika maeneo yao ya kazi na kwingineko.

 Malengo ya Mafunzo haya kwa Mafundi ni :-
    Kujenga na kuongeza ufahamu na utaalam wa fundi katika fani yake
    Kumuongezea uwezo wa kufanya kazi yake kwa wepesi na ubunifu
    Kufanya mazingira ya kazi kuwa rafiki kwa kufuata sheria na masharti ya usalama kazini
    Kutambua namna mbadala ya kufanya kazi zake huku akipunguza matumizi ya vifaa (materials) yasio ya lazima na hivyo kupunguza gharama za ujenzi
    Kuhakikisha kazi inafanywa  kwa  Ubora na kiwango  stahiki ili kuhimili ushindani katika soko
    Kupembua na kutoa maamuzi sahihi  yanapohitajika katika utekelezaji wa kazi zao
    Kutunza muda pindi atekelezapo majukumu yake
    Kufanya eneo lake la kazi kuwa safi wakati wote wa ufanyaji kazi

Mafundi watakapokamilisha mafunzo yao  hupewa vyeti  na  wasifu wao kuhifadhiwa katika rekodi ya  chama kama mafundi  waliohitimu na kufudhu katika fani husika.

Hivyo mbali na kampuni kunufaika na  kazi zenye viwango  kwa gharama ya chini lakini pia utakuwa umemuongezea fursa fundi huyu kuendelea kuboresha sekta ya ujenzi kwingineko hivyo kufanya kandarasi za wazawa zizidi  kukua na kuthaminiwa na jamii yetu.

Mafunzo haya huwa ni madaraja matatu (3) ambapo mafunzo ya mwanzo fundi hutunikiwa cheti cha nyota moja, mafunzo ya awamu ya pili fundi hutunikiwa cheti cha nyota mbili na mafunzo ya awamu ya tatu fundi hutunukiwa cheti cha nyota tatu na kuonesha amefudhu mafunzo hayo na anaweza  kuwa mwalimu  kwa mafundi wengine wa fani yake.

Hivyo chama kinatoa fursa hii kwa makandarasi kuleta mafundi wao katika fani ya  Plastering & Tiles Layer.

Mafunzo yataanza Tarehe 10 hadi 22 July, 2017 katika kituo chetu cha Mafunzo kilichopo Arusha Technical College - Arusha.

Gharama ya Mafunzo ni Tsh. 300,000/= kwa Wanachama wa ACCT na Tsh. 400,000/= kwa Wasio wanachama .

Gharama hizi za ushiriki ni kwa ajili  Vifaa vya kufundishia,  Chai  ya asubuhi na Chakula cha Mchana.  

Gharama  nyingine kama usafiri na kujikimu zitakuwa juu ya kampuni ya mshiriki au mtu binafsi mwenyewe.

Nafasi ni chache, hivyo  makandarasi  wazawa mnaombwa kutumia fursa hii  ambayo italeta  mapinduzi na tija kwa kazi za wazawa.

Tafadhali  thibitisha ushiriki wako kwa kututumia jina  na mawasiliano ya Fundi/Mshiriki   kupitia  simu namba 0762 074 441 au  Email: info@acct.co.tz ili uweze kutumiwa fomu ya kujiunga (Joining Instruction)

Wote mnakaribishwa

BI. ANGELA JOSEPH
KATIBU MTENDAJI
 
Association of Citizen Contractors Tanzania (ACCT);
Sinza B; Mbutu street Plot no. 55; Block 4
P.O Box 14666; Dar es salaam; Tanzania;
Contact; +255 762 074 441
Email: info@acct.co.tz; angela.joseph@acct.co.tz,
Website: www.acct.co.tz